Friday 25 September 2009

WATARUDI KUJA KUCHUKUA WAKE ZAO.

Na. Deborah Robert

Habarini za siku ndugu zangu, wakubwa zangu shikamooni. Namshukuru Mungu kwa nguvu na uweza wake kunifanya mzima wa afya mpaka leo hii ninapofurahia kuongea nanyi.

Pamoja na kwamba hatujazungumza kwa muda mrefu ninayo mengi sana ya kuwaeleza, maana nimetembea kwingi na nina habari nyingi. Na leo napenda kuongeea na wasichana wenzangu ambao hatujaolewa.

Msichana ninaye taka kumzungumzia leo ni yule aliyekwisha balehe, tena mwenye haraka ya kutaka kuolewa kwa kuwa tu takwimu ya Taifa inasema wanawake ni wengi kuliko wanaume.

Kutokana na hali hiyo basi imekuwa kasumba kwetu sisi wadada kutongoza na kutaka kuolewa haraka bila hata ya kuchukua muda kufahamiana zaidi na yule amtakae, ili mradi tu awahi chake mapema.

Hili limekuwa tatizo katika ndoa nyingi sana hapa kwetu maana zimekuwa ndoa za wenda kuangalia mkato wa chumba tu na baada ya wiki, mwezi au mwaka ndoa hiyo huvunjika.

Inauma sana wapendwa wangu maana wanaume wamekuwa kama wacheza kamali na kujivuna kuwa wanao uwezo wa kuwa na wanawake zaidi maana wanawake ni wengi tena wengi wanadai uwiano wa mume mmoja ni wanawake watatu.

Hatupo tayari kudhalilishwa hivyo, tena napinga kwa herufi kubwa HATUTAKI. Kama kwa Afrika wanaume ni wengi basi Marekani ni wachache na wao mwatarudi kuja kuchukua wake zao Tanzania.

Maana asili ya mmarekekani ni hukuhuku kwetu Afrika. Watarudi tuu!!!

Kuzaliwa msichana sio laana, tujitambue kuwa tupo na tunaweza kuungana na kutoa kauli yetu ya kupinga hali hii ili sisi basi tupate nafasi ya kujiendeleza kimasomo na kuchagua tuwapendao kuishi nao baada ya kufahamiana.

Nawambia wapendwa wangu hakuna mtu mmbaya hapa duniani, heee! Aliyesema we mbaya nani? Kwanza hata uwezo wa kukuumba upya hana. Jitambue msichana!!!

Hii ilikuwa ni moja ya changamoto iliyojadiliwa kwenye Kongamano la wasichana katika Maadhimisho ya miaka 50 ya YWCA yaliyofanyika Moshi, Tanzania kwa muda wa wiki moja kuanzia tarehe 13/9/09 mpaka 17/09/09.

Kwaherini!!!!

Maoni yanakaribishwa!!!

No comments: