Friday 23 October 2009

MAMBO YETU YALE!!!!


TWINS WITH THEIR KAKA


Katikati ni kaka yangu jamani, pembeni ni pacha wangu katika graduation yangu - TUMAINI UNIVERSITY IRINGA

DEGREEEEEEEE!


NELLY


Headgirl wa Ashira Secondary aliyefahamika kwa jina moja NELY alipanda mti kuwakilisha wanafnzi wenzake.

Rais wa YWCA Kenya naye alipata nafasi ya kupanda mti.


UDONGO MGUMU HUU!!

Raisi wa YWCA Tanzania Mrs Rosemary Mapagala akipanda mti shule ya Wasichana Ashira katika maadhimisho ya miaka 50 ya YWCA Tanzania.

PANDA MTI BABA

Mkuu wa bodi ya Shule ya wasichana Ashira akipanda mti shuleni hapo ikiwani ishara ya kuadhimisha miaka 50 ya YWCA Tanzania yaliyofanyika Moshi.

Wednesday 21 October 2009

JAMANI NIMEGRADUATE


"Kwa mamlaka niliyopewa nakutunuku shahada ya kwanza ya UANAHABARI wewe DEBORAH ROBERT na MUNGU akubariki" alisema ALEX MALASUSA mkuu wa vyuo vya Tumaini Tanzania.

Sunday 11 October 2009

UTAMBULISHO

Rais wa Young Women Christian Association, Mrs. Rosemary Mapagala ambaye aliingia madarakani mwaka huu baada ya kustaafu kwa Miss Joyce Sabuni Mukoji. Rais akiwasalimu washiriki na wanafunzi wa Ashira Secondary. Kushoto kwake ni Rais wa YWCA ya Kenya na kulia kwake ni Mkuu wa shule ya Ashira.
Katibu mkuu wa YWCA ya Tanzania Mrs. Loerose Mbise akitambulisha meza kuu na wageni aliotangulizana nao.

TUNAINGIA UWANJANI

Wanafunzi wa kidato cha tano HGL wakiingia kwa kuimba wimbo wa pongezi ambao ulichanganyika na beat ya wimbo mmoja wa marehemu Michael Jackson.

MKUU WA SHULE.

Mkuu wa shule ya wasichana Ashira akiwakaribisha wageni ambao ni viongozi na wanachama wa YWCA katika maadhimisho ya miaka 50 ya TYWCA.

Friday 9 October 2009

WIMBO WA SHULE

Wanafunzi wa Ashira Secondari wakiimba wimbo wa shule yao, Shule kwa ajili ya kutengeneza viongozi waadilifu na wajasiri.

Thursday 8 October 2009

Miaka 50 ya YWCA Tanzania

Wanachama wa YWCA walipowasili Ashira Secondary School kwa kuanza maadhimisho hayo yaliyochukua wiki moja wilayani MOSHI.

Friday 25 September 2009

Wanafunzi wa Ashira Girls

Nasisi tutakuwa member wa YWCA, Wanafunzi wakijiandaa kupokea wageni wa YWCA ikiwa ni maadhimisho ya miaka 50. Tulikwenda Ashira ikiwa ni kumbukumbu ya na kuenzi mahali hapo ambapo YWCA ilianzishiwa hapo.

WATARUDI KUJA KUCHUKUA WAKE ZAO.

Na. Deborah Robert

Habarini za siku ndugu zangu, wakubwa zangu shikamooni. Namshukuru Mungu kwa nguvu na uweza wake kunifanya mzima wa afya mpaka leo hii ninapofurahia kuongea nanyi.

Pamoja na kwamba hatujazungumza kwa muda mrefu ninayo mengi sana ya kuwaeleza, maana nimetembea kwingi na nina habari nyingi. Na leo napenda kuongeea na wasichana wenzangu ambao hatujaolewa.

Msichana ninaye taka kumzungumzia leo ni yule aliyekwisha balehe, tena mwenye haraka ya kutaka kuolewa kwa kuwa tu takwimu ya Taifa inasema wanawake ni wengi kuliko wanaume.

Kutokana na hali hiyo basi imekuwa kasumba kwetu sisi wadada kutongoza na kutaka kuolewa haraka bila hata ya kuchukua muda kufahamiana zaidi na yule amtakae, ili mradi tu awahi chake mapema.

Hili limekuwa tatizo katika ndoa nyingi sana hapa kwetu maana zimekuwa ndoa za wenda kuangalia mkato wa chumba tu na baada ya wiki, mwezi au mwaka ndoa hiyo huvunjika.

Inauma sana wapendwa wangu maana wanaume wamekuwa kama wacheza kamali na kujivuna kuwa wanao uwezo wa kuwa na wanawake zaidi maana wanawake ni wengi tena wengi wanadai uwiano wa mume mmoja ni wanawake watatu.

Hatupo tayari kudhalilishwa hivyo, tena napinga kwa herufi kubwa HATUTAKI. Kama kwa Afrika wanaume ni wengi basi Marekani ni wachache na wao mwatarudi kuja kuchukua wake zao Tanzania.

Maana asili ya mmarekekani ni hukuhuku kwetu Afrika. Watarudi tuu!!!

Kuzaliwa msichana sio laana, tujitambue kuwa tupo na tunaweza kuungana na kutoa kauli yetu ya kupinga hali hii ili sisi basi tupate nafasi ya kujiendeleza kimasomo na kuchagua tuwapendao kuishi nao baada ya kufahamiana.

Nawambia wapendwa wangu hakuna mtu mmbaya hapa duniani, heee! Aliyesema we mbaya nani? Kwanza hata uwezo wa kukuumba upya hana. Jitambue msichana!!!

Hii ilikuwa ni moja ya changamoto iliyojadiliwa kwenye Kongamano la wasichana katika Maadhimisho ya miaka 50 ya YWCA yaliyofanyika Moshi, Tanzania kwa muda wa wiki moja kuanzia tarehe 13/9/09 mpaka 17/09/09.

Kwaherini!!!!

Maoni yanakaribishwa!!!

Thursday 24 September 2009

SAFARI YANGU YA MOSHI - ASHIRA

JAMANI NIMEWAMISSSSSSSSSS!!!!! DU NILIKUWA BUSY KISHENZI NA SHULE NDO IMEISHA.
heshima zenu wadau wangu, na wadogo nipeni basi haki yangu, du kweli mna haki ya kunishtaki!!!
Sasa nimerudiii!!
Safari yangu nilikuwa Moshi kwenye Maadhimisho ya miaka 50 ya YWCA. Du kweli wanawake tukiwezeshwa tunaweza sana tu.
Katika maadhimisho haya wapendwa tulitembelea shule ya wasicha ASHIRA ambako Shirika la YWCA lilipoanzia.
Usiondoke wala usibadili web endelea kufurahia.

Monday 27 October 2008

Miaka 30 ya ndoa ya Mchungaji Kakusi!

Mwaka 1978 ilikuwa ni nderemo na vifijo pale ambapo Mchungaji Jackson Kakusi na Bi Sabina Kakusi wa Moravian Kigoto Mwanza walipouvua ukapela na kuwa kitu kimoja. Nderemo hizo zimejirudia tena mwaka huu ambapo imetimu miaka 30 ya ndoa hiyo.

Friday 24 October 2008

Nimerudi! Mnisamehe sana wadau!

Kwanza kabisa mimi nahitaji msamaha wenu kwa kukaa kimya muda mrefu! Wapenzi wangu nilikuwa nimetightiwa sana na masomo lakini kwa sasa namshukuru Mungu kwani yeye pekee ndiye muweza wa yote aniwezeshaye kufanya mengi mnayoyaona leo.

Nawaahidi kuwa kwa sasa nimerudi kuwapatia kile ambacho ni halali yenu kupata ambacho ni habari katika picha.

Asanteni kwa kunvumilia na kunitumia comments zatu za kunijulia hali na maisha kwa ujumla.

KARIBUNI TULE NA KUNYWA PAMOJA KATIKA MEZA HII YA UANAHABARI>

Tuesday 7 October 2008